Waziri
mkuu mwanzilishi wa Singapore, Lee Kuan Yew amefariki dunia.Lee
amefariki akiwa na umri wa miaka tisini na mmoja kutokana na ugonjwa wa
mapafu.
Kwa miongo mitatu ya utawala wa Lee alifanikiwa kuipitisha
nchi yake katika kipindi cha mpito na kuleta mabadiliko makubwa ya
kiuchumi hasa katika usafirishaji majini kwa kutumia rasilimali kidogo
walizokuwa nazo na sasa kuwa kitovu kikubwa cha kibiashara cha
kimataifa.
David Adelman ni balozi wa zamani wa Marekani nchini
humo, ametuma salamu zake za rambi rambi.Kifo cha Lee ni mwisho wa zama
zake.mwisho wa mwanamume mwenye nguvu ya ushawishi aliyeingia madarakani
katikati ya miaka ya sitini .
Lee alifanikiwa kuanzisha
ushirikiano wa kirafiki kati ya nchi yake na Marekani ambao umedumu hata
leo na unaweza kuvuka mipaka sio kwa singapore tu bali hata kwa watu wa
Asia ya kusini Mashariki.
0 comments:
Post a Comment