Pages

Home » » MAHAKAMA YA MWANZO MWANJELWA YAELEMEWA NA KESI ZA MIRATHI, TAKALA NA MADAI

MAHAKAMA YA MWANZO MWANJELWA YAELEMEWA NA KESI ZA MIRATHI, TAKALA NA MADAI


Hakimu wa mahakama ya mwanzo Mwanjelwa JP MWAMBAPA ameitaka jamii kutumia mabaraza ya kata na mitaa katika kusuhisha kesi za kifamilia na madai ili kutoa nafasi kwa mahakama kusikiliza kesi ambazo zimekuwa vigumu kuamriwa na mabaraza hayo.

Aliyasema hayo wakati wa mahojiano na mtandao huu ofisini kwake na kudai kuwa kesi nyingi zimekuwa zikishindwa kufikiwa muafaka kutokana na wanafamilia wenyewe kushindwa kuyatumia mabaraza ya kata.

Aidha MWAMBAPA alizitaja baadhi ya kesi zinazoongoza kusikilizwa mahakamani hapo kuwa ni kesi za mirathi, talaka na madai ambapo kwa sehemu kubwa zimekuwa ni vigumu kutolewa hukumu kutokana na walalamikaji kutopitia kwenye mabaraza ya kata pamoja na vyombo vya dini.

Hata hivyo alisema chanzo cha kesi hizo ni mmomonyoko wa madili ndani ya jamii.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

1 comments:

Home Magazine said...

Itasaidia kupunguza kwa mrundikano wa kesi mahakamani na kusikilizwa kwa wakati muafaka na kuepusha rushwa!!

Post a Comment

 
Support : Greyson Salufu | Chimbuko Letu Inc | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Mbwile Media - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger