Pages

Home » » WAWILI WAFA KATIKA MATUKIO MAWILI TOFAUTI NA MMOJA AJERUHIWA KWA AJALI YA MOTO

WAWILI WAFA KATIKA MATUKIO MAWILI TOFAUTI NA MMOJA AJERUHIWA KWA AJALI YA MOTO

Na.Gabriel Mbwille.




Watu wawili wamefariki dunia katika matukio mawili tofauti akiwemo MAGRETH MWAKASEGE mwenye umri wa miaka 36 aliyefariki dunia kwa kuungua moto na kusababisha majeruhi kwa mtu mmoja wakati wakiwa wamelala nyumbani kwao.

Akiongelea matukio hayo Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya BARAKIEL MASAKI alisema tukio hilo limetokea jana majira ya saa tano za usiku kata ya Ilemi mtaa wa Mapelele na kusema kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme.

Aidha alimtaja aliyejeruhiwa kuwa ni MAWAZO MWAKASEGE mwenye umri wa miaka 39 ambaye ni mume wa marehemu na yupo katika hospitali ya rufaa kwa ajali ya matibabu

Wakati huohuo kamanda MASAKI alisema watu wasiofahamika wamevunja kanisa la UYOLE CHRISTIAN FELLOWSHIP na kuiba vitu vyenye thamani ya shilingi million 8 majira ya saa tano na dakika 20 usiku maeneo ya uyole mtaa wa sokoni.

Aliongeza kuwa jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa kuwabaini waliohusika na tukio hilo la wizi na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano na Jeshi la polisi ili kufanikisha kuwatia mbaroni watuhumiwa hao.





Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Greyson Salufu | Chimbuko Letu Inc | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Mbwile Media - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger