Serikali ya mpito ya Somalia itakabidhi madaraka kesho kwa serikali
ya kudumu baada ya kuongoza nchi hiyo kwa kipindi cha miaka 8.
Bunge la Somalia linatazamiwa kuchagua rais mpya wa nchi hiyo kesho na
kukabidhi madaraka ya nchi kwa serikali ya kudumu. Habari zinasema
serikali ya mpito ya Somalia mbayo imekuwa madarakani tangu mwaka 2004
itajiuzulu kesho na kukabidhi madaraka kwa serikali mpya. Serikali hiyo
ya mpito inakosolewa kwamba haikuweza kurejesha amani kamili nchini
Somalia katika kipindi cha miaka 8 iliyopita.
Rais wa serikali ya mpito inayomaliza muda wake Sheikh Sharif Sheikh
Ahmad, Waziri wake Mkuu Abdiweli Muhammad Ali na Spika wa Bunge la
Somalia Sharif Hassan Sheikh Adam wanagombea kiti cha rais katika
uchaguzi wa kwanza wa kisiasa wa Somalia tangu miaka 20 iliyopita.
NEW VIDEO:- CHRIS BEE - SIENDI MBALI
5 years ago
0 comments:
Post a Comment