Daladala likizimwa moto na kikosi cha moto Iringa
Daladala yenye namba T 717 AWK mali ya Ayubu Kabigi ikiwaka moto eneo la mshindo.
Na: Denis Mlowe - Iringa
Zaidi
ya abiria 20 wanusurika kufa katika ajali ya gari aina ya daladala
inayofanya shughuli za kusafirisha abiria kati ya Mkwawa na Kihesa
Kilolo baada ya daladala hiyo kuungua moto na kuteketea kabisa chanzo
kikiwa ni hitilafu katika mfumo wa injini.
Ajali
hiyo iliyotokea mida ya saa saba mchana ilihusisha daladala aina
ya kipanya yenye namba T 717 AWK mali ya Ayubu Kabigi ilitokea katika
maeneo ya Mshindo karibu kabisa na kituo cha mafuta cha Sherry na Kanisa
kongwe la Mshindo mkoani hapa.
Shuhuda
ya ajali hiyo Anthony Zamilinga amesema kwamba gari hiyo ilikuwa
ikitokea maeneo ya Mwangata ilipofika sehemu ya tukio alimwona dereva
akishuka na kuanza kuchukua mchanga kwa lengo la kupambana na moto
uliokuwa ukianza kuwaka na ulipozidi baadhi ya abiria wakaanza kuruka
katika gari hiyo na
kupiga simu katika kikosi cha zima moto kilichofika haraka eneo la
tukio na kuzima katika gari hilo licha ya kuungua na kuteketea kabisa.
Msemaji wa Zimamoto Kaimu Mkuu wa Kituo Sajenti Meja John Zakaria amesema chanzo cha ajali hiyo hitalafu ya umeme iliyotokea katika gari hiyo na kuwataka wamiliki wa vyombo vya usafiri kuwa na tabia ya kuwa na vifaa vya kuzimia moto katika magari yao. “kikosi cha zimamoto kinatoa elimu kila mara kuhusu elimu ya kukabiliana na majanga ya moto na kuna namba za simu za dharura ambazo ziko wazi wakati wote lakini wananchi hawana tabia ya kutoa taarifa mapema na ndio maana hasara kama hizi zinajitokeza hivyo hatuwezi kuota kama kuna janga la moto hivyo naomba ushirikiano wa wananchi katika majanga ya moto kama haya” alisema Sajenti Meja Zakaria

Mmiliki
wa dala dala hiyo Ayubu Kabigi amesema kwamba amepata hasara ya sh
milioni 8 kutokana na ajali hiyo na amewashukuru sana wananchi
waliojitokeza kusaidia kuzima gari yake kwani wakati anapigiwa simu
alikuwa anajiandaa na safari ya nje ya mkoa. “nawashukuru sana wananchi
wa maeneo ya mshindo na kikosi cha zimamoto kuwahi kufika mara baada ya
kupewa habari kuhusu janga hilo licha ya kwamba gari lilikuwa limewaka
moto na kuteketea” alisema Kabigi
0 comments:
Post a Comment