Chama
cha waandishi wa habari za UKIMWI Tanzania (AJAAT) kwa kushirikiana na
Tume ya Kudhibiti UKIMWI nchini (TACAIDS) kinatangaza shindano kwa
wanahabari kuhusu kuzuia maambukizo ya VVU na UKIMWI kwa vijana na
wanawake. Shindano hili linadhaminiwa na Mfuko wa Umoja wa Mataifa
unahusika na ongezeko la watu (UNFPA).
Likiwa na kichwa cha habari cha:
Shindano la wanahabari kuhusu madhara na juhudi za kuzuia VVU na UKIMWI
kwa Vijana na Wanawake, shindano hili linalenga kuwaunganisha wanahabari
wote kuandika kuhusu madhara ya VVU na UKIMWI kwa vijana na wanawake,
na ni kitu gani kifanyike kuzuia makundi haya mawili dhidi ya maambukizo
mapya na hatimaye kuwa na familia bora na taifa imara kwa ujumla.
Shindano litakalodumu kwa miezi mitatu, kuanzia Desemba 31, 2012 hadi Machi 31, 2013, litawahusisha wandishi watanzania wa magazeti, Runinga, Redio na Mitandao ya kijamii (hususani bloggers).Kimsingi, shindano hili linalenga kuwawezesha wanajamii kutambua na kuwahamasisha kujikita katika juhudi zitakazosaidia taifa kufikia mpango na mkakazi wa kupunguza maambukizo ya VVU na kufikia maambukizo sifuri ifikapo mwaka 2015. Mkakati huu ni sehemu ya shughuli ya Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa kwa Tanzania (UNDAP 2011-2015) katika mpango mkakati wake wa kila mwaka, wa Mpango la Umoja wa Mataifa, kikundi kazi cha VVU na UKIMWI.
Maudhui ya makala au vipindi vitakavyokubaliwa kushindanishwa lazima vijikite katika kuonyesha jinsi VVU na UKIMWI ulivyowaathiri vijana na wanawake kiuchumi, kijamii na hali ya afya zao kwa ujumla. Habari zitakazo andikwa kwa mfano, lazima zionyeshe au kutoa mwanga juu ya maswala muhimu kama vile uzuiaji wa VVU miongoni mwa vijana na wanawake, utoaji huduma kwa vijana au wanawake wanaoishi na VVU, matibabu, huduma kwa familia zilizoathirika sana, upatikanaji wa rasilimali, utafiti na ufahamu wa mambo yanayohusu VVU miongoni mwa jamii. Makala lazima zieleze kwa nini kwa mfano, makundi haya mawili yameendelea kuwa katika hatari zaidi ya kuambukizwa VVU na UKIMWI nchini, na sababu zake ni nini hasa.

Makala au vipindi hivi lazima vitoe
ushauri au vionyeshe njia muafaka za kuzuia maambukizo ya VVU kwa
kuwalenga vijana na wanawake.
2.0 Wanaotakiwa kushiriki na Vigezo vyake:
Washiriki wa shindano
ni waandishi wanaondika au kutangaza katika vyombo vya habari vya hapa
nchini au wageni wanafanyakazi katika vyombo vya habari vya Tanzania
Vitu vitakavyoruhusiwa
kushindanishwa ni makala, program za TV na Radio, Vibonzo, picha na
habari zilizochapishwa katika blogs.
Makala au habari au kibonzo kitakachoshindanishwa lazima kilenge mambo kama vile unyayapaa na ubaguzi, kwa nini vijana na wanawake wapo katika hatari zaidi ya kuambukiizwa VVU, changamoto zinazowapata vijana na wanawake katika kupata taarifa za VVU, huduma na misaada mingine kwa wanaoishi na VVU, habari hizi lazima ziandikwe au kutangazwa kwa kwa kina na ziwe na uwezo wa kuelemisha.
Makala lazima zilenge na kuelemisha jamii ya kitanzania
Makala au vipindi
lazima ziwe au viwe halisia na zisinakiliwe kutoka sehemu yoyote kama
vile kutoka kwenye magazeti, Majarida, Runinga, Vipindi vya radio,
mitandao ya kijamii n.k.
Makala
itakayoshindanishwa lazima iwe imetoka kwenye gazeti au chombo chochote
cha habari kati ya Desemba 31, 2012 na Machi 31, 2013.
Lugha inayokubalika kutumiaka katika makala au vipindi zitakazoshindanishwa ni Kiswahili na Kiingereza.
Ni makala halisi zisizonakiliwa kutoka chombo cha habari kingine zitakazo kubaliwa na kupokelewa.
Idadi ya makala au vipindi vinavyoruhusiwa kushindanishwa kutoka kwa mwandishi mmoja ni tatu (3).Tarehe ya mwisho ya kutuma/kuwasilisha na kupokelewa nakala za kushindanisha ni Aprili 7, 2013
Zawadi mbalimbali za
kuvutia ikiwa ni pamoja na vyeti vitatolewa kwa washindi ambao
watachaguliwa na jopo la majaji weredi kutoka tasnia za afya, masauala
ya VVU/UKIMWI pamoja na vyombo tofauti vya habari.
3.0 Walengwa:
Wandishi wa habari wa Tanzania
kutoka vyombo vyote vya habari—runinga, redio, magazeti, wapiga picha,
wachora vibonzo na wandishi wa mitandao ya kijamii (bloggers)
4.0 MUDA WA SHINDANO:
Desemba 31, 2012 hadi Machi 31, 2013
5.0 KUTUMA NAKALA YA KUSHINDANISHA:
Tuma nakala za makala zako za kushindanisha au zipeleke kwa mkono kwa:
Bi. Jovina Bujulu
Idara ya Habari MAELEZO,
Samora Avenue
DAR ES SALAAM
AU
Zitume kwa njia ya Posta au kwa mkono kupitia:
SHINDANO LA MAKALA ZA VVU NA UKIMWI KWA WANDISHI WA HABARI,
SHINDANO LA AJAAT-UNFPA-TACAIDS,
S.L. P 33237, KIJITONYAMA, BAHARI MOTORS BLDG.
KITALU NA.43, DAR ES SALAAM AU PIGA SIMU: 0713 640520/0786 300219/ 0786 653712,
Imetolewa na
A Simon Kivamwo
Chairman, AJAAT
0 comments:
Post a Comment