EDDO MAKATA MWAMALALA
Gabriel Ernest.
MWANASHERIA Eddo Makata Mwamalala, ametangaza rasmi kuachana na chama cha
demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa madai kuwa amechoshwa na kuchonganishwa
na jamii na kutakiwa kuandika barua ya kuomba kugombea Ubunge 2015 makao makuu.
Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ukumbi wa Mbeya Peack
Jijini Mbeya leo, Mwamalala ambaye alikuwa katibu wa Chadema mkoa wa Mbeya na
Mjumbe wa mkutano mkuu Taifa, alisema kuwa hivi karibuni kuna viongozi wamejitosa
kumshambulia baada ya yeye kutimiza wajibu wake wa kikatiba wa kumtaka katibu
mkuu wa chgama hicho taifa kujiuzulu baada ya kukiri kumiliki kadi ya CCM.
‘’Leo tarehe 03/01/2012
ni siku muhimu yenye kumbukumbu nyingi juu ya maisha yangu kisiasa.
Kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA ya mwaka 2006 kipengele cha 5.4 kukoma kwa
Uanachama, kifungu kidogo cha 5.4.1; nanukuu “ kwa kujiuzulu mwenyewe kwa hiari yake.” Mimi Edo
Makata Mwamalala leo hii naamua kutekeleza katiba hiyo; najiuzulu uanachama’’
alisema Mwamalala.
Alizitaja baadhi ya
sababu za kuachana na chama hicho kuwa ni pamoja na kutokubaliana na Dr. Slaa
kuwa na kadi ya CCM, matumizi ya Ruzuku si sahihi, huku Maafisa wa makao Makuu wakiishi
kama wafalme na Malkia na kuwafanya wanachama wa Mikoani kama kuku wa kienyeji
kwa kuwarushia punje za mchele unapotaka kuwachinja.
‘’Mikoani viongzi na
wanachama wanatoa pesa zao kwa kujichangisha kwa imani kuwa siku moja
watakula keki ya Ruzuku na ufadhili. Mimi nawahakikishia , kwa
unyenyekevu nilioufanya hawatopata hadi Mbowe na Slaa watoke kwenye
nafasi walizo nazo kwa sasa,wasidanganywe na siasa za mikutano ya matumaini ya
kitaifa yenye posho’’ alisema Mwamalala.
Mbali na sababu hizo
alitanabaisha kuwa sababu nyingine ya kuachana na Chadema ni mchakato wa
mgombea uraisi (2010) ndugu Slaa kamati kuu ilipendekeza jina lake
na kuitisha Baraza kuu bila kuwasikiliza viongozi wenmgine wa
mkutano mkuu na sasa hivi mwanachama anayetaka kugombea jimbo anatakiwa
kuandika barua makao Makuu.
‘’Huu ni utawala
wa ki-ubwenyenye ndani ya chama kuwafanya wapinzani wako
wakudhuru au wakuzidi kete kwa mbinu za kujuana makao Makuu na Kitendo
cha mwenyekiti wa chama Mhe,Freeman Aikael Mbowe (Mb) kiongozi wa kambi Rasmi
ya upinzani kuropoka, eti Ndugu Slaa atakuwa ndiye ngombea uraisi
mwaka 2015 ni cha kuua kabisa Demokrasia ndani ya Chadema’’
‘’Tena
ninamshauri bure kakangu ninayemheshimu kwa siasa zake; atubu kama aliwahi
kumshambulia Yusuf Makamba alipokuwa katibu mkuu – CCM aliposhilia bango, kuwa
mgombea mwenye mtaji ni Jakya Kikwete. Mbowe awaombe radhi wanachama na
wananchi wapenda mabadiliko. Hawezi kuwaburuza wasomi kama prof. Baregu,
Prof. Safari, Dk. Kitila Mkumbo na wengine wengi’’ alisema Mwamalala.
Alisema
yeye angeulizwa kuwa nani anafaa kuiendesha Chadema ngazi ya Taifa angemtaja
Dk. Kitila kuwa awe katiba mkuu wa chama hicho hata kuingizwa kwenye
mchakato wa ugombea nafasi za juu za nchi.
‘’Pia ndani ya Chadema kuna
migogoro isiyo na suluhu wa mlingano katika kuitatua, Mfano ni Mwanza na Arusha,
chama kimefukuza Madiwani, lakini Karatu nyumbani kwa Dr. Slaa wanabembelezwa,
hapa pana ajenda ya kuifanya Chadema iwe ni SACCOS tu huku maandamano
ya kudai haki’’
‘’Hata siku moja
hayajaitishwa Moshi, Karatu ili nako wananchi wa kule waonje joto ya jiwe
kupambana na polisi, Maandamano ni Mbeya, Mwanza, Arusha ambako viongozi wao
wanafukuzwa wakiongea ukweli au kutoa hoja zenye mantiki’’ alisema Mwamalala
0 comments:
Post a Comment