Mkurugenzi wa Maendeleo na Utamaduni wa Wizara ya Habari Bw. Herman
Mwasoka (mwenye suti nyeusi) akimfariji Baba mzazi wa Marehemu Sajuki
Mzee Juma Kilowoko alipofika nyumbani kwa marehemu kuhani msiba huo
Tabata Bima jijini Dar.
Mkurugenzi
wa Utamaduni na Maendeleo wa Wizara ya Habari Bw. Herman Mwasoka akitia
saini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu Sajuki jijini Dar
leo.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Bi. Joyce Fisso akitia saini kitabu cha maombolezo ya Msiba wa Sajuki.
Msanii mkongwe katika tasnia ya muziki wa Dansi na Rhumba Kikumba Mwanza
Mpango almaarufu kama King Kiki akitia saini kitabu cha maombolezo
nyumbani kwa Marehemu Sajuki Tabata Bima jijini Dar leo.
Mzee
King Kiki akiteta jambo na Mkurugenzi wa Utamaduni na Maendeleo wa
Wizara ya Habari Bw. Herman Mwasoka (katikati) nyumbani kwa marehemu
Sajuki jijini Dar leo. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini
Bi. Joyce Fisso
Wasanii
mbalimbali na wakiendelea kuwasili nyumbani kwa Marehemu Sajuki Tabata
Bima jijini Dar es Salaam. Pichani ni Msanii wa muziki Dokii (kushoto)
sambamba na Mshiriki wa Shindano la Big Brother Africa Mwisho Mwampamba
na wasanii wengine.
Mchekeshaji
maarufu wa The comedy Masanja Mkandamizi akijifuta jasho kwa mbali
akielekea msibani nyumbani kwa Marehemu Sajuki. Masanja alikuwa ni mmoja
wa wahamishaji katika kuchangia pesa za matibabu ya marehemu Sajuki
kwenda nchini India kupitia kipindi cha Luninga cha The Comedy
kinachorushwa na Televisheni ya TBC.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa kwenye huzuni kutafakari kifo cha Sajuki.
VIONGOZI
WA SERIKALI WAKIWASILI: Mbunge wa jimbo la Segerea, Dar es Salaam,
ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga (wa
tatu kushoto) akiwa ameambatana na Mbunge wa jimbo la Kinondoni Mh.Iddi
Azzan wakipokelewa na Rais wa Shirikisho la Filamu nchini (TAFF) Bw.
Simon Mwakifamba na wasanii wengine wa filamu baada ya kuwasili nyumbani
kwa Marehemu Sajuki kwa ajili ya kuhani msiba huo.
Mkuu
wa Itifaki Bw. Simon Simalenga wa Clouds Media akimuongoza Mh.Makongoro
Mahanga sehemu maalum kwa ajili ya kutia saini kitabu cha maombolezo.
Mbunge
wa jimbo la Segerea, Dar es Salaam, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi
na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga akitia saini katika kitabu cha
maombolezo nyumbani kwa marehemu Sajuki.
Mbunge wa Kinondoni Mh. Iddi Azzan naye aliangusha saini kwenye kitabu hicho.
Mzee King Kiki akizungumza jambo na Waheshimiwa Wabunge kwenye msiba wa Sajuki Tabata Bima jijini Dar es Salaam leo.
Waheshimiwa
wakielekea nyumba ya jirani walikokusanyika baadhi ya waombolezaji na
wasanii wa filamu nchini kwa ajili ya kuzungumza machache na kutoa
Ubani.
Katibu
wa Fedha msibani hapo mchekeshaji maarufu Steve Nyerere akiwakaribisha
waheshimiwa wabunge kuzungumza na hadhira ya waombolezaji (hawapo
pichani).
Mbunge
wa jimbo la Segerea, Dar es Salaam, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi
na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga akitoa salamu zake za rambimbi na
kuahidi kuchangia shilingi 200,000/= kwa ajili ya kufanikisha shughuli
za mazishi ya mpendwa wetu Marehemu Sajuki atakayezikwa Kesho Ijumaa
katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Mbunge
wa jimbo la Kinondoni Mh. Iddi Azzani akielezea kwa majonzi alivyopokea
taarifa za msiba wa Sajuki na kuahidi kushirikiana bega kwa bega na
Wastara panapomajaliwa ya Mola katika malezi ya mtoto aliyeachwa na
marehemu na kuwaasa wadau, ndugu, jamaa na marafiki kumsaidia Wastara
kutokana na hali yake na amechangia kiasi cha Shilingi 500,ooo/=
kufanikisha shughuli za mazishi ya marehemu Sajuki.
Pichani
Juu na Chini ni Umati wa waombolezaji ukisikiliza nasaha za waheshimiwa
Wabunge (hawapo pichani) walipofika nyumbani kwa marehemu Sajuki kuhani
msiba huo.
Kazi
ya kuosha vyombo si kina Dada tu, hata kina Kaka wanaweza pia….Pichani
ni baadhi ya Watangazaji wa Clouds Radio wakiongozwa na Dina Marios
kushiriki kuosha vyombo vilivyotumika katika msiba huo huku wakisaidiana
na waombolezaji wengine.
Mganga
wa Jadi anayefahamika kwa jina la Dokta Manyaunyau (kushoto) sambamba
na Msanii wa filamu nchini Cloud wakisikiliza mawaidha ya waheshimiwa
wabunge (hawapo pichani).
Mkuu
wa Itifaki msibani hapo Bw. Simon Simalenga wa Clouds Media akimpokea
Mwenyekiti wa kamati ya Kusaidia timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys
Bw. Ridhiwani Kikwete alipowasili nyumbani kwa marehemu Sajuki kwa ajili
ya kuhani maeneo ya Tabata Bima jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa kamati ya Kusaidia timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys Bw.
Ridhiwani Kikwete akitoa pole baada ya kusaili kwa baadhi ya ndugu wa
karibu wa marehemu Sajuki msibani hapo.
Bw.
Ridhiwani Kikwete akisalimiana na Baba mzazi wa marehemu Sajuki Mzee
Juma Kilowoko nyumbani kwa marehemu Tabata Bima jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa kamati ya Kusaidia timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys Bw.
Ridhiwani Kikwete akitia saini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa
marehemu Sajuki leo.
Bw. Ridhiwani Kikwete akimpa maneno ya faraja Baba mzazi wa Marehemu Sajuki Mzee Juma Kilowoko.
Bw. Ridhiwani Kikwete akitoa mkono wa pole kwa mke wa marehemu Sajuki Bi. Wastara (mwenye buibui).
Bw. Ridhiwani Kikwete akimfariji mama mzazi wa Marehemu Sajuki alipofika nyumbani hapo kuhani msiba huo.
Katibu wa fedha msibani hapo Steve Nyerere akitetea jambo na Bw. Ridhiwani Kikwete.
Rais
wa Shirikisho la Filamu nchini (TAFF) Bw. Simon Mwakifamba akizungumza
machache kabla ya kumkaribisha Bw. Ridhiwani Kikwete kuzungumza machache
na waombolezaji.
Mwenyekiti
wa kamati ya Kusaidia timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys Bw.
Ridhiwani Kikwete akizungumzia marehemu Sajuki na kuwataka wanawake
kuiga mfano wa Maisha ya Sajuki na Wastara jinsi walivyokuwa wakiishi na
Upendo mpaka Umauti ulipomkuta marehemu Sajuki na kuwasisitiza kuenzi
yale yote mema aliyokuwa akifanya kipindi cha uhai wake na kuwamasisha
Umoja na Mshikamano baina yao.
Bw.
Ridhiwani Kikwete naye alichangia Shilingi 500,000/= kwa ajili ya
kufanikisha mazishi ya Mpendwa wetu Sajuki anayetarajiwa kuzikwa Kesho
Ijumaa katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Pichani Juu na Chini ni Baadhi ya wasanii wa filamu wakisikiliza nasaha za Bw. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani).
Marehemu
Sajuki alikuwa kipenzi cha watoto na wakubwa pia. Pichani ni Umati wa
watoto wanaokaa jirani na Nyumba ya Marehemu Sajuki wakiwa wamekusanyika
huku wakionyesha majonzi na simanzi tele.
0 comments:
Post a Comment