MBWA wa kiraia 12 kutoka katika maeneo mbalimbali
ya jijini Mbeya wamepatiwa mafunzo na jeshi la polisi ya kupambana na wezi
na vibaka ili kuimarisha ulinzi.
Mafunzo yametolewa na jeshi la polisi mkoani Mbeya katika
kitengo cha mafunzo ya farasi na Mbuwa ambapo wamepatiwa mafunzo jinzi ya
kumtambua mwizi na jinsi ya kumkamata.
Akifunga mafunzo hayo ya mbwa kaimu kamada wa polisi mkoa
wa Mbeya, Barakael Masaki alisema mafunzo hayo yatakuwa chachu ya ulinzi
shirikisha kwani sasa mafunzo hayo ni ya kwanza kwa mbwa wa kiraia.
Alisema mafunzo hayo yatakuwa chachu kwa raia wengine
wenye mbwa kupeleka mbwa wao kupata mafuzo hayo ya ulinzi salama majumbani
mwao.
Masaki aliongeza kuwa jeshi hilo limekuwa likitoa mafuzo
ya mbwa kwa miaka mingi japo kuwa wananchi walikuwa hawatambui kutolewa kwa
mafuzo hayo ya kisasa.
Alisema mafinzo ya mbwa kuwa ni ajira kama ajira zingine
kwa wale waloo peleka mbwa wao katika mafunzo watakuwa babarozi wazuri na kuwa
waalimu kwa wenzao.
Alisema kuwa mbwa wanaakili kama za binadamu kwani
anafundishika kama akielewa nini cha kufanya na hutekeleza kile anacho elekezwa
na hufanya kwa umakini.
Alisema mbwa aliyepatiwa mafunzo anaweza kuwa mlinzi
salama na anaweza kupunguza gharama za kuajili walinzi majumbani kama ukiwanae.
Mafunzo hayo yalifungwa mwishoni mwa mwaka jana ambapo
mafuzo yalidumu kwa muda wa miezi milili kuanzia Novemba mosi hadi Disemba 31
mwaka jana, pia mbwa hao walicheza gwalide wakiongozwa na askali wa jeshi la
Polisi.
Alisema mafuzo hayo ya mbwa 12 yamegharamiwa na jeshi la
polisi ambapo kutakuwa na mafuzo mengine ambayo yatagharamiwa na mwenyembwa na
zitatolewa fomu za kuandikisha mbwa watakao patiwa mafuzo nakuwa wananchi
watatanzaziwa itakapofika wakati wa kuandikisha.
Mbwa hapo pia watatumiwa na jeshi la polisi katika kusaka
wahalifu endapo utatokea katika maeneo waliopo mbwa hao ambapo kama ujharifu
utatokea katika kata ambayo kuna mbwa akali wata mfuata mbwa aliyepata mafunzo
na kuwasaka waharifu.
0 comments:
Post a Comment