IMANI za kishirikina zimezidi kukitisa Kijiji cha
Isange na Kata ya Isange baada ya matukio ya kupotea na kuawa kwa Watoto
kutokea mara kwa mara ambapo Marehemu hukutwa wakiwa na mapungufu ya viungo
ikiwemo Kichwa.
Katika tukio la hivi karibuni Mtoto mmoja
aliyejulikana kwa Jina la Lista Sebule (8) Mwanafunzi wa Darasa la Saba
katika Shule ya Msingi Mpombo iliyo katika Kata ya Isange
Halmashauri ya Busokelo Wilaya ya Rungwe Mkoani hapa ambaye alipotea katika
mazingira ya kutatanisha na kukutwa baada ya Siku 9 akiwa amekufa.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo akiwemo
Mama mzazi wa Marehemu Christina Sakalile alisema binti yake alipotea majira ya
saa tisa jioni Machi 31, Mwaka huu baada ya kutumwa kupeleka simu kibandani ili
kuchaji lakini hakurudi hadi Saa Kumi na Mbili jioni hali iliyozua wasiwasi na
kuanza kumtafuta bila mafanikio.
Alisema baada ya tukio hilo walitoa taarifa
Kijijini ambapo Mwenyekiti wa Kitongoji cha Isange Daudi Nsyani ambaye baada ya
kupewa taarifa hizo pia aliwataarifu viongozi wa Kata akiwemo Diwani wa Kata ya
Isange Elias Mwasandele na Ofisa Mtendaji wa kata hiyo Brayson Nguro ambaye
aliitisha Mkutano wa wananchi.
Mtendaji huyo aliwaambia wananchi hao
kushirikiana ili Mtoto apatikane hali ambayoiliitikiwa na wananchi ambayo
walitaka Mtoto apatikane aidha akiwa mzima ama Mfu ambapo juhudi za kumtafuta
zilianza na hatimaye kumpata Aprili 8, Mwaka huu akiwa amekufa huku akiwa hana
baadhi ya Viungo.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema Mwili wa
Marehemu ulipatikana ukiwa pembezoni ya Mto Nkalisi uliopo Kijijini hapo ukiwa
umenyofolewa baadhi ya viungo kama Kichwa na Miguu ambapo mguu mmoja
ulipatikana baada ya Mbwa kukutwa akiwa ameshika na kuudondosha baada ya
kukutana na watu hali iliyowalazimu watu hao kumfutilia Mbwa huyo aliyeongoza
hadi Mwili wa Marehemu ulipokuwepo na kuwakuta Mbwa wengine wawili wakiwa
pembezoni.
Baada ya kupatikana kwa mwili huo Taarifa
ilipelekwa Polisi ambao walifika katika eneo la tukio na kuupima kisha
kuwakabidhi ndugu kwa ajili ya mazishi ambapo watu wawili walikamatwa
kuhusika na tukio hilo baada ya kupigiwa kura za siri na wananchi na kukutwa na
kura nyingi ambapo wengine wanne waliachiwa kutokana na kutokuwa na kura
nyingi.
Kutokana na hali hiyo Ofisa Mtendaji wa kata hiyo
alisema mfululizo wa vitendo hivyo unatokana na kutokuwa na Vituo vya Polisi
ambapo Halmashauri ya Busokelo inakituo kimoja kilichopo katika Mji wa Lwangwa
mahali ambapo ni mbali sana kutokana na gharama kuwa kubwa.
Kwa upande wake Diwani wa kata hiyo Elias
Mwandele alisema wananchi waache kutembea usiku ambapo aliongeza kuwa Vilabu
vya Pombe kufungwa saa mbili usiku huku akiwataka Wazazi kutowapeleka watoto
kwenye Shughuli za Machungo ambapo wameweka ulinzi wa Sungusungu ili kudhibiti
hali hiyo.
|
0 comments:
Post a Comment