Na Benedict Liwenga, Maelezo, Dodoma.
Jumla ya Watanzania 342 wamepata fursa ya kusoma masomo mbalimbali nje
ya Tanzania kati ya mwaka 2010 hadi 2012. Kauli hiyi imetolewa leo
Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mhe.
Philipo Augustino Mulugo wakati akijibu swali la
Mbunge
wa Jimbo la Gando, Mhe. Khalifa Suleiman Khalifa aliyetaka kujua ni
vijana wangapi wamepata nafasi za masomo nje ya nchi kuanzia mwaka
2010-2012 na ni vijana wangapi kutoka Zanzibar pamoja na nchi gani
walikwenda kusoma.
Mhe.
Mulugo amesema kuwa katika kuwapatia ufadhili unaotolewa na vijana
wanashindanishwa kwa kutumia vigezo vya kitaaluma, umri na uraia wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aidha,
ameongeza kuwa kinachozingatiwa zaidi ni kigezo cha kitaaluma, mwombaji
yoyote anayetimiza kigezo hicho anayo haki ya kunufaika na ufadhili bila
kujali anatokea sehemu gani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mhe.Mulugo
amebainisha kuwa kutokana na mwingiliano wa wananchi wa pande mbili za
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inakuwa vigumu kutofautisha sehemu ya
Jamhuri alipotokea muombaji.
“Napenda
kusisitiza kuwa nafasi za masomo zinatolewa kwa ajili ya wananchi wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwamba wote wanashindanishwa kwa
vigezo vya kitaaluma na si vinginevyo.
Katika
kipindi cha mwaka 2010 hadi 2012, nchi ambazo zimekuwa zikitoa nafasi za
masomo kwa Watanzania nje ya nchi ni Cuba, Algeria, Urusi,
Msumbiji,Serbia, Uingereza, Misri, Korea Kusini, Macedonia, Uturuki,
China, Ujerumani na Oman.
0 comments:
Post a Comment