Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akizundua bohari ya madawa ya MSD mjini Dodoma Mei
5,2013.Wapili kulia ni Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Seif RashidWatatu
kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Bohari ya Madawa (MSD), Cosmas Mwaifani.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akikata utepe wakati alipozindua bohari ya kuhidi
madwa ya MSD, eneol la Kizota mjini Dodoma Mei 5,2013.Kulia ni Naibu
Waziri wa Afya, Dkt. Seif Rashid na Kushoto ni Kaimu Mwenyekiti wa Bodi
ya Wadhamini ya MSD, Malima Lubeleje. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa
Bohari ya Madawa (MSD), Cosmas Mwaifani (wapili kulia) wakati
alipozinduaghala la kuhifadhia madawa katika Kanda ya Kati la MSD mjini
Dodoma Mei 5, 2013. Katikati ni Naibu Waziri wa Afya, Dr. Seif Rashid
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akikagua madawa yaliyohifadhiwa kwenye boahari ya
MSD ya Kanda ya Kati eneo la Kizot mjini Dodoma baada ya kuzindua
bohari hiyo Mei 5,2013. Wapili Kulia ni Naibu Waziei wa Afya, Dkt.Seif
Rashid , Kushoto ni Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MSD,
Malima Lubeleje na wapili kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa MSD, Cosmas
Mwaifani. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
…………………………………………………….
WAZIRI
MKUU Mizengo Pinda amemwagiza Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,
Dk. Seif Rashid awasiliane na Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ili watafute njia ya kuinusuru Bohari ya
Dawa (MSD).
Amesema
hawana budi kutafuta njia ya kuhakikisha kuwa asilimia 67 inayotengwa
na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) kwa ajili ya kulipia dawa za wagonjwa
mbalimbali inatumiwa ipasavyo na si vinginevyo.
Ametoa
kauli hiyo leo mchana (Jumapili, Mei 5, 2013) wakati akizindua ghala
jipya la kisasa la kuhifadhia dawa lililojengwa na Bohari ya Dawa, Kanda
ya Dodoma huko Kizota, nje kidogo ya mji wa Dodoma.
Ujenzi
wa ghala hilo ambao umegharimu sh. bilioni 9.9/-, umechangiwa na
Serikali ya Marekani kupitia Shirika lake la USAID na Mfuko wa Kimataifa
wa Kupambana na UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria (Global Fund).
0 comments:
Post a Comment