Hali ya eneo mlipuko ulipotokea Waumini na wananchi wengine wakiwa na shauku ya kujua kilichotokea Ulinzi umeimarishwa Viongozi wa Kanisa wakitoa taarifa ya kilichotokea kwa waandishi wa habari kabla ya Balozi wa Papa kuondolewa Kanisani hapo chini ya ulinzi mkali wa Polisi. Wanasualama Mkoa wa Arusha, wakijadiliana jambo katika eneo la tukio Meya wa Manispaa ya Arusha, Mh gaundence Lyimo akielekea eneo la tukio kwa miguu baada ya utaratibu wa kutumia magari kuwa mgumu kutokana na idadi kubwa ya watu na magari yaliyoziba njia. Magesa Mulongo akiteta na RCO wa Mkoa wa Arusha Mkuu wa Mkoa wa Arusha, magesa Mulongo akijiandaa kuzungumza na wananchi kanisani hapo na kuahidi kuwa Serikali itahakikisha watu wote waliohusika na jaribio hilo ovu, pamoja na mtandao wao wanakamatwa. Alidai pia vikosi vya Jeshi maalumu kwa kuchunguza milipuko vitafika eneo hilo ili kufanya uchunguzi. Taarifa za eneo la tukio zinaeleza kuwa tayari kuna mshukiwa mmoja ameshatiwa mbaroni na yuko mikononi mwa Jeshi la Polisi kwa mahojiano na uchunguzi zaidi. Eneo lenye utepe ndipo kitu hicho kinachodhaniwa kuwa bomu kilipoangukia. Pichani unaweza kuona wigi za kichwani na viatu vya waumini vikiwa vimesambaa baada ya wenyewe kuviacha, miongoni mwao wakiwa ni majeruhi. Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo akizungumza na mmoja wa mapadri wa Kanisa hilo kupewa maelezo ya kuhusu kilichotokea kanisani hapo.
RPC- ARUSHA ATHIBITISHA KUWA KILICHOLIPUA KANISA NI BOMU....
WATU 3 WANAHALI MBAYA, 50 WAMEJERUHIWA
RPC wa mkoa wa Arusha naye
aliambatana na mkuu wa mkoa na muda huu alikuwa anatoa nasaha
zake kwa wananchi....
RPC ameeleza kuwa tukio hili ni la kigaidi. Katika maelezo yake, RPC amesema kuwa aliyehusika alijitokeza nyuma ya
jengo kwa kujificha na kurusha bomu. ...
Amesema Polisi wanawasaka waliohusika na unyama huu na ameomba yeyote mwenye taarifa yoyote aisaide polisi. ..
Waliojeruhiwa ni 50 .Hao wana majeraha ya kawaida na 3 wako mahututi
Mpaka sasa mtu mmoja anashikiliwa na polisi kwa
mahojiano zaidi
0 comments:
Post a Comment