Pages

Home » » Askari 57 wa Marekani waingia Syria

Askari 57 wa Marekani waingia Syria


Duru za habari zinaarifu kuingia nchini Syria askari 57 waliostaafu wa Marekani kwa ajili ya kuwasaidia magaidi wanaotekeleza mauaji na uharibifu nchini humo. 

Shirika la Habari la Fars limeripoti kuwa maafisa hao 57 waliwasili nchini Uturuki na ndege ya Kimarekani ya C-130 na kuingia Syria kupitia njia ya mkoa wa mpakani wa Reyhanlı. Aidha ndege hiyo ilikuwa imebeba pia zana za kijasusi kwa ajili ya kuwasaidia magaidi. 
Wakati hayo yakiripotiwa, kikao cha siku ya Jumamosi cha nchi zinazojiita eti marafiki wa Syria kilichofanyika mjini Doha, Marekani na baadhi ya nchi za Magharibi ikiwemo Uturuki, Qatar na Saudia, zilikubaliana kuongeza misaada yao kwa wapinzani wa Syria na makundi ya kigaidi yenye mafungamano na kundi la kigaidi la Al-Qaida. 
Wakati huo huo, magaidi ambao wanaonekana kushindwa na jeshi la serikali halali ya Rais Bashar al-Assad wa nchi hiyo, wameanzisha wimbi jipya la kuwashambulia ovyo raia wasio na hatia wa nchi hiyo, ili kwa njia hiyo waweze kuishinikiza serikali ya Damascus. 
Weledi wa masuala ya kisiasa wa Mashariki ya Kati wanaamini kuwa, kikao cha Doha, Qatar hakikufanikiwa na kwamba, ni mwanzo wa kushindwa.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Greyson Salufu | Chimbuko Letu Inc | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Mbwile Media - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger