Mwanamke mkulima mkazi wa kijiji cha
Kisana wilaya ya Iramba mkoa wa Singida Sayuni Ramadhani (42), amehukumiwa
adhabu ya kutumikia jela miaka mitatu baada ya kukiri kosa la kumng’ata uume
mume wake, Onesmo Nathania (42), na kubakia ngozi ndogo, nusura
ukatike.
Mwendesha
mashitaka mkaguzi wa polisi Vicent Ndasa, alidai mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama
ya wilaya ya Iramba Mrisho Mrisho, kuwa mnamo Juni 4 mwaka huu saa 12.00 jioni
huko katika kijiji cha Kisana, mshitakiwa kwa makusudi aling’ata kwa nguvu uume
wa mume wake na kumsababishia maumivu makali.
Ndasa amesema siku ya tukio, wanandoa hao waliporejea nyumbani kutoka kwenye klabu ya pombe za kienyeji mali ya kijiji cha Kisana, kulitokea kutokuelewana na kupelekea waanze kugombana.
Ndasa amesema siku ya tukio, wanandoa hao waliporejea nyumbani kutoka kwenye klabu ya pombe za kienyeji mali ya kijiji cha Kisana, kulitokea kutokuelewana na kupelekea waanze kugombana.
Amesema
wakati wanaendelea kupigana, Onesmo alizidiwa nguvu na aliangushwa chini kisha
kugandamizwa na zipu yake ya suruali kufunguliwa na mshitakiwa ambaye
baadaye alifanikiwa kuutoa uume wa mumewe kutoka ndani ya nguo ya ndani na
kuutia mdomoni na ksiha kuung’ata kwa nguvu.
Mwendesha mashitaka huyo, amesema kuwa mlalamikaji, Onesmo alipiga yowe na majirani wema walifika mara moja na kisha kumkimbiza katika zahanati ya kijiji kwa ajili ya matibabu.
Mwendesha mashitaka huyo, amesema kuwa mlalamikaji, Onesmo alipiga yowe na majirani wema walifika mara moja na kisha kumkimbiza katika zahanati ya kijiji kwa ajili ya matibabu.
Kabla
ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Ndasa aliiomba mahakama hiyo impe adhabu kali
mshitakiwa ili iwe fundisho kwake na kuogofya wanawake wanaotarajia kuwafanyia
unyama wa aina hii waume zao ukome.
Kwa
upande wake, mshitakiwa Sayuni aliiomba mahakama hiyo imwonee huruma na kumpa
adhabu nafuu kwa madai kuwa hilo
ni kosa lake la kwanza toka amezaliwa na vile vile ana jukumu kubwa la
kushirikiana na mume wake katika kulea idadi kubwa ya watoto walionao.
Akisoma
hukumu hiyo, hakimu mfawidhi Mrisho, alisema mahakama yake imezingatia kwa
makini maombolezo ya mshitakiwa na kufikia uamuzi wa kutoa adhabu ya kutumikia
kifungo cha kwenda jela miaka mitatu.
0 comments:
Post a Comment