Pages

Home » » TANZANIA IMEKUWA TISHIO KWA VITENDO VYA KIKAILI, MFANYAKAZI WA JAJI KILEO AMCHINJA MFANYAKAZI MWENZAKE WA KIKE RAIYA WA KENYA

TANZANIA IMEKUWA TISHIO KWA VITENDO VYA KIKAILI, MFANYAKAZI WA JAJI KILEO AMCHINJA MFANYAKAZI MWENZAKE WA KIKE RAIYA WA KENYA

MFANYAKAZI WA JAJI KILEO AMCHINJA MFANYAKAZI MWENZAKE WA KIKE RAIYA WA KENYA


KAMANDA SULEIMAN KOVA
Baada ya jana mtandao huu wa thesuperstatz kuripoti juu ya msichana mrembo kukutwa jalalani akiwa amechinjwa na watu wasiojulika .kwasasa jeshi la polisi limeanza kupata mwanga mara baada ya kumshikilia philemon Laiza ambaye amekiri kuhusika na tukio hilo  hii hapa ni taarifa kamili.

MFANYAKAZI wa Jaji Kileo, Philemon Laiza (27) anadaiwa kumchinja mtumishi wa ndani wa jaji huyo, ambaye ni raia wa Kenya, Perpetua Mainab (30). Mtuhumiwa huyo, ambaye alikuwa ni mtunza bustani katika nyumba ya Jaji Kileo, alifanya unyama huo wiki iliyopita. Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Kamishna wa Polisi Kanda Maalum, Suleiman Kova, alisema mwili wa mtumishi huyo wa ndani ulikutwa kwenye dampo la kutupia takataka maeneo ya Mikocheni B.

“Tukio hilo lilitokea karibu na dampo la kutupia taka Mikocheni ‘B’, katika eneo linalomilikiwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).

“Mfanyakazi huyo wa ndani alikutwa ameshakufa baada ya mwili wake kuchinjwa sehemu ya shingo, jeraha sehemu ya mkono wa kushoto karibu na kiganja, jeraha kwenye paji la uso na mwili wake ukiwa umetapakaa damu sehemu za kichwani,” alisema Kova.

Alieleza kuwa mtuhumiwa huyo ambaye alikuwa akifanya kazi pamoja na marehemu, alikiri kuwa na marehemu siku hiyo ya Ijumaa ya Juni 8 mwaka huu.

Alisema baada ya polisi kufanya upelelezi mtuhumiwa alikutwa na kiatu kimoja cha marehemu na nguo alizovaa siku ya tukio, ambazo zilikuwa zimetapakaa damu.
MWILI WA MAREHEMU PEPETUA ALIYEKUWA MFANYAKAZI WA JAJI KILEO UKIWA UMETUPWA JALALANI KAMA TAKA MARA BAADA YA KUCHINJWA KAMA KUKU
Mwili wa Pepetua Maina ukiwa katika shimo la taka.
MREMBO aliyejulikana kwa jina la Pepetua Maina au maarufu kama Lucy, Mkikuyu wa Kenya anayekadiriwa kuwa na miaka 25 mpaka 30 amekutwa amekufa kwa kuchinjwa shingo na mwili wake kutupwa katika shimo la taka.
 
 Mwili wa huo ulikutwa na polisi Juni 8, mwaka huu  Mikocheni B, jirani kabisa na makazi ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova.

Kwa mujibu wa mtoa habari, mwili wa msichana huyo ulionekana na mfanyakazi mmoja wa ndani wakati akienda kutupa takataka eneo hilo ambapo alipouona alipiga kelele zilizowafanya majirani kukimbilia eneo la tukio na kujionea wenyewe.
...Mwili wa Pepetua baada ya kufunikwa.
Taarifa za kipolisi zilidai kuwa mrembo huyo kabla ya kuchinjwa alipigwa kwani mkono mmoja wa kushoto ulivunjika na kukutwa na jeraha kubwa katika paji la uso.
Wakizungumza na Uwazi kwa tahadhari kubwa kuogopa ushahidi, baadhi ya majirani wa eneo hilo walisema hawakusikia vurugu zozote usiku kwa hiyo huenda wauaji walimchinja mbali na kwenda kuutupa mwili wake eneo hilo.
Mwili wa Pepetua ukitolewa shimoni na polisi.
Juni 9, mwaka huu, Uwazi lilizungumza na Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Dar es Salaam, ACP Camillius Wambura kuhusu kifo cha msichana huyo ambapo alikiri kutokea.
Kamanda Wambura alisema kuwa, Pepetua alikuwa akifanya kazi kwa Jaji Engera Kileo kwa miaka mitatu mpaka siku ya kifo chake.
Mwili wa Pepetua baada ya kutolewa shimoni.
“Jeshi la polisi tulipokea habari za kuwepo kwa mwili huo jana (Jumamosi) saa sita na nusu, tukaenda na kuukuta ukiwa kwenye shimo la taka umechinjwa shingoni na kiganja cha kushoto kilikatwa na kitu chenye ncha kali na kwenye paji la uso alipasuliwa.
...Mwili wa marehemu ukiingizwa kwenye gari.
“Tuliuchukua na kwenda kuuhifadhi Hospitali ya Mwananyamala. Vijana wawili wanaoishi kwa Jaji Kileo ndiyo waliofika hospitali na kumtambua marehemu. Jaji mwenyewe alikuwa safarini nje ya nchi, amerejea leo (juzi Jumapili). “Mpaka sasa tunamshikilia mtu mmoja kwa mahojiano kuhusiana na kifo hicho, siwezi kuzungumza kwa undani zaidi,” alisema Afande Wambura.

“Nguo hizo za marehemu zilikuwa zimetapakaa damu na baada ya mahojiano ya muda mrefu, mtuhumiwa alikiri kuhusika na tukio hilo. Kamishna Kova alisema kuwa mtuhumiwa alipohojiwa alidai kuwa marehemu alitoweka nyumbani tangu siku ya Ijumaa na baada ya kubanwa na polisi mtuhumiwa alikiri kuhusika na tukio hilo.
Kova alisema mtuhumiwa bado anahojiwa na upepelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani. Katika tukio jingine, jeshi hilo lilifanikiwa kuwakamata majambazi nane wanaojihusisha na uporaji mali za raia wa kigeni katika fukwe ya Bahari ya Hindi.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Greyson Salufu | Chimbuko Letu Inc | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Mbwile Media - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger