Pages

Home » » MATUKIO YA UBAKAJI WA WATOTO NI TATIZO MBEYA

MATUKIO YA UBAKAJI WA WATOTO NI TATIZO MBEYA


Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, mtuhumiwa alitenda kosa hilo usiku wa June 11, 2013 wakati mama mzazi wa mtoto huyo akiwa kirabuni anauza Pombe.

mmoja wa wakazi wa Kijiji cha Kisegese Anywelwisye Mwasomola Aliiambia Mbwile Media kuwa mtuhumiwa Imanuel Kajuki baada ya kuona mtoto huyo akiwa peke yake nyumbani kwao ndipo alipoamua kumvutia chumbani kwake na kuanza kumwingilia kimwili.
"Unajua nini kaka wakati tukizungumza na mtoto huyo aliyebakwa alisema kuwa Ima alimvutia chumbani kwake na kuanza kumvua nguo kisha kuanza kumwingilia kimwili na kadili alipojaribu kupiga kelele bado kijana huyo aliendelea kumfanyia kitedo hicho"alisema Mwasomola.

Kwa upande wake mama mdogo wa mtoto huyo ambaye jina lake tunalihifadhi kwa sababu za kimaadili alisema kuwa mtuhumiwa baada ya kutenda tukio hilo alitorokea kusikojulikana hata hivyo taarifa tayari zimekwisha fikishwa katika ofisi ya kata kwa hatua zaidi za kisheria

Naye mganga mfawidhi wa kituo cha afya Kandete DrSuleiman Idi Mhina alisema muathiriwa wa tukio hilo la ubakaji alifikishwa katika kituo hicho majira ya saaa moja za asubuhi na kwamba uchunguzi wa awali umeonysha mtoto huyo alianza kuingiliwa lakini mtuhumiwa hakufanikisha kutimiliza adhma yake kikamilifu huku akiongeza kuwa huduma ya kwanza ilitolwa kwa mtoto huyo kuanza kupewa huduma za kujikinga na magonjwa ya ngono

Hata hivyo mwenyekiti wa kijiji hicho Isa Mwemsi aligoma kuongelea tukio hilo huku akidai kuwa hana taarifa ya kutokea kwa tukio hilo
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Greyson Salufu | Chimbuko Letu Inc | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Mbwile Media - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger